MBEYA-Benki Kuu ya Tanzania imeendesha semina ya mafunzo kwa Watoa Huduma Ndogo za Fedha Daraja la Pili iliyofanyika jijini Mbeya tarehe 24 hadi 27 Septemba 2025.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watoa huduma ndogo za fedha wa daraja la pili ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo mbalimbali iliyotolewa na Benki Kuu katika kusimamia biashara ya huduma ndogo za fedha daraja la pili.