BUKOMBE-Wananchi wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita wameonesha mshikamano mkubwa na nia thabiti ya kuendeleza juhudi za maendeleo kwa kutangaza wazi msimamo wao wa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika uchaguzi ujao wa Oktoba.
Wakiwa wamejipanga kwa kauli mbiu isemayo “Oktoba Tunatiki!”, wananchi hao pia wametangaza kuwa wanamuunga mkono Dkt. Doto Mashaka Biteko, wakimtaja kama chaguo sahihi kwa maendeleo ya Bukombe kutokana na uongozi wake thabiti,wa wazi na wa kisera.
Aidha, wananchi hao wameahidi kuwatiki madiwani wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakieleza kuwa wana imani na ilani ya chama hicho pamoja na utekelezaji wake katika ngazi zote za serikali.
Kauli mbiu kama
#ChaguaCCM,
#ChaguaSamia,
#ChaguaBiteko,
#OktobaTunatiki,
#KusemaNaKutenda,
na
#KaziNaUtuTunasongaMbele zimeendelea kushika kasi katika majukwaa mbalimbali ya kijamii na mikutano ya hadhara, zikionesha ari ya wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia huku wakitazamia maendeleo endelevu.
