CCM Kileleni,Dkt.Mwinyi avutiwa na kasi ya kampeni zikiashiria ushindi wa kishindo

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi leo Septemba 8, 2025 amekutana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt.Asha Rose Migiro, Ikulu Zanzibar.
Dkt.Mwinyi amempongeza Dkt.Migiro kwa uteuzi wake wa kuwa Katibu Mkuu CCM Taifa na kueleza matumaini yake makubwa kutokana na uwezo wake, huku akifurahishwa na mwenendo wa kampeni za CCM unaoashiria kukubalika kwa Chama na ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Aidha, amemtakia mafanikio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kushukuru CCM Makao Makuu kwa msaada wake kuelekea uzinduzi wa kampeni Zanzibar Septemba 13,2025.
Naye, Katibu Mkuu Dkt. Migiro ameahidi kushirikiana na CCM Zanzibar na kufanya kazi bega kwa bega katika kampeni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news