ZANZIBAR-Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kinatarajia kufungua rasmi kampeni zake za uchaguzi Septemba 13,2025 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Uzinduzi huo unatarajiwa kuwa tukio kubwa lenye kuvutia hadhira ya maelfu ya wanachama wa CCM na wananchi wapenda maendeleo kutoka pande zote za visiwani kutokana na kazi kubwa iliyofanyika katika kipindi cha miaka mitano chini ya Mheshimiwa Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
Hatua hii ni muhimu katika kuendelea kuimarisha mshikamano wa wanachama, wananchi na kuonesha uongozi unaoacha alama chini ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Mgombea Urais, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
