DCEA yawakamata wahandisi wanaotengeza Biskuti za bangi Mbeya

NA GODFREY NNKO 

MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imewakamata Henry Shao (36) na Veronika Samumba (31) wakiwa na biskuti 241 zilizotengenezwa kwa bangi mkoani Mbeya.
"Watajwa ni wahandisi na wafanyakazi wa kampuni binafsi za ujenzi za HSS Engineering Company Limited na JIC Company Limited za jijini Mbeya."

Hayo yamesemwa leo Septemba 8,2025 jijini Dar es Salaam na Kamishna Jenerali wa DCEA,Aretas Lyimo wakati akizungumza na waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari.
"Baada ya upekuzi eneo la Mtaa wa Forest watuhumiwa walikutwa na vifaa wanavyovitumia kutengeza biskuti hizo na kueleza kwamba wateja wao wakubwa ni wahandisi na vijana wa vyuo na mitaani."

Kamishna Jenerali Lyimo amesema, mamlaka hiyo inaendelea kuvunja mitandao ya dawa za kulevya na kubaini mbinu mpya za biashara na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo kuongeza wigo wa utoaji elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya.

Amesema,lengo ni kuakisi dhamira ya Taifa katika kulinda usalama wa wananchi na kuimarisha uchumi, kujali utu, kulinda afya za watanzania, hatimaye kujenga jamii imara kwa ustawi wa Taifa letu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news