GEITA-Bodi ya Bima ya Amana (DIB) imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu jinsi inavyokinga amana za wateja wa benki na taasisi za fedha katika Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan mjini Geita.
Pichani, wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Bugando wakipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma na Mawasiliano wa Bodi hiyo, Bw. Lwaga Mwambande.
Maonesho ya Teknolojia ya Madini yalianza tarehe 18 Septemba na yanatarajiwa kufungwa tarehe 28 Septemba,2025.
Tags
Bodi ya Bima ya Amana (DIB)
Deposit Insurance Board
(DIB)
Habari
Maonesho ya Madini Geita
The Deposit Insurance Board (DIB)








