Dkt.Mwinyi kuzindua Kampeni za CCM Pemba leo

ZANZIBAR-Mgombea wa kiti cha Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameondoka Unguja leo Jumatatu, tarehe 15 Septemba 2025 na kuwasili Kisiwani Pemba kwa ajili ya Uzinduzi wa Kampeni za CCM.
Dkt. Mwinyi amewasili katika Uwanja wa Gombani ya Kale, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba, ambako ndiko kumeandaliwa uzinduzi rasmi wa Kampeni za CCM kwa upande wa Pemba.
Uzinduzi huu unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, viongozi wa Chama na Serikali, pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii, huku Dkt. Mwinyi akitarajiwa kueleza dira na vipaumbele vya CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news