Na Derek K. Murusuri
Dar es Salaam
Septemba 29,2025
MWELEKEO wa Sekta ya Madini nchini Tanzania tangu mwaka 2021 ni kielelezo cha mafanikio makubwa ya Falsafaya 4R katika kuunda uchumi imara unaotabirika, ulio wazi na wenye tija.
Kabla ya kipindi hiki, sekta hii ilikumbwa na mazingira ya magumu na migogoro ya kodi isiyoisha.
Uhasama wa kisiasa ulikwamisha mitaji ya ndani na nje. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani, alifanya mageuzi makubwa kwa kutumia nguzo za Maridhiano na Mageuzi ili kuboresha mazingira ya kufanya biashara nchini. Utulivu mkubwa ukatamalaki na mafanikio katika sekta ya madini yakaleta neema nchini.



