NA LWAGA MWAMBANDE
ALPHONCE Felix Simbu leo Septemba 15,2025 ameweka historia baada ya kuwa mwanariadha wa kwanza kutoka Tanzania kushinda medali ya dhahabu katika Mashindano ya Dunia ya World Athletics Championship 2025 huko Tokyo nchini Japan.
Katika mashindano hayo, Simbu alikimbia kwa kasi ya hali ya juu, akimshinda kwa tofauti ndogo sana Amanal Petros wa Ujerumani.
Wote walimaliza kwa muda sawa wa saa 2:09:48, lakini baada ya mfumo bunifu wa kuweka muda kiotomatiki ulioundwa ili kupima kwa usahihi utendaji wa riadha (photo finish) kuangaliwa kwa makini, Simbu alitangazwa mshindi kwa sekunde 0.03 pekee.
Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anabainisha kuwa, huu ni ushindi wa kihistoria kwa Tanzania, kwani ni mara ya kwanza mshindi wa dhahabu kutoka Tanzania katika mashindano hayo Dunia. Endelea;
1. Mwanariadha mahiri, umetikisa dunia,
Ulivyofanya vizuri, ushindi kujipatia,
Shangwe kubwa siyo siri, na sifa kwa Tanzania,
Hii kapeti nyekundu, anastahili Simbu.
2. Marathoni kuwapiga, mbio ulivyotimua,
Sasa twaenda kwa swaga, jinsi umetuinua,
Shampeni tunazimwaga, ubingwa tumeujua,
Hii kapeti nyekundu, anastahili Simbu.
3. Sijaelewa vizuri, au niseme sijui,
Sababu na sifa nzuri, kuzidi la nazi tui,
Wanaofanya vizuri, wapasayo siyajui,
Hii kapeti nyekundu, anastahili Simbu.
4. Hii kapeti nyekundu, ile ya waheshimiwa,
Wenye vyeo kama nundu, kote wanatambuliwa,
Ni kwa kazi si utundu, hao wanainuliwa,
Hii kapeti nyekundu, anastahili Simbu.
5. Mwaka ishirina mbili, kwa michezo ya Madola,
Vema aliikabili, wala hatukuchalala,
Aliibeba medali, ikaja hadi Ilala,
Hii kapeti nyekundu, anastahili Simbu.
6. Hati nzuri zile kubwa, kupita VIP,
Ile ya watu wakubwa, kwani Simbu hafikii,
Kafanya mambo makubwa, heshima kwa nchi hii,
Hii kapeti nyekundu, anastahili Simbu.
7. Si mtu wa kawaida, jinsi abeba taifa,
Duniani ambeshinda, yake mengi maarifa,
Chati nchi ishapanda, ameleta yeye sifa,
Hii kapeti nyekundu, anastahili Simbu.
8. Mwanariadha mahiri, vema kumlinganisha,
Na wa zamani mahiri, ambao walitingisha,
Kuileta histori, vema hawa kukumbusha,
Hii kapeti nyekundu, anastahili Simbu.
9. Suleiman Nyambui, alitamba enzi hizo,
Ni nani hamtambui, Bayi wa kwake uwezo,
Sasa nchi maadui, twawaweza kimichezo,
Hii kapeti nyekundu, anastahii Simbu.
10. Simbu Mwakilishi wetu, ulichofanya hongera,
Sifa kubwa nchi yetu, muda watu kuwakera,
Walotuona si kitu, kwenye mbio hizi bora,
Hii kapeti nyekundu, anastahili Simbu.
11. Pia napendekeza, mtu huyu kumuenzi,
Sanamu kutengeneza, akiwa afanya kazi,
Hiyo izidi pendeza, vizazi hata vizazi,
Hii kapeti nyekundu, anastahili Simbu.
12. Nadhani hata kazini, hili watalitambua,
Pale ameketi chini, wazidishe kumwinua,
Mepanda yake thamani, na nchi kaiinua,
Hii kapeti nyekundu, anastahili Simbu.
Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602