Madhehebu ya dini ni nguzo ya amani nchini-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema madhehebu ya dini yana mchango mkubwa katika kudumisha amani na utulivu wa Taifa.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo leo wakati akihutubia Kongamano la Kuiombea Nchi Amani lililoandaliwa na Umoja wa Akina Mama wa Kikristo na Maendeleo Zanzibar, Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema amani ni neema inayopaswa kuenziwa na kila mmoja, huku akisisitiza wajibu wa viongozi wa dini kuwaelimisha waumini kuhusu umuhimu wa amani.

Halikadhalika, amewahakikishia akina mama wa Kikristo kuwa Serikali itaendelea kushughulikia changamoto za taasisi za dini ili ziweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news