Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 zimeendelea wilayani Karagwe ambapo Mwenge huo umefanya uzinduzi, uwekaji wa jiwe la msingi na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 3.58 tarehe 12 Septemba 2025.
Miradi iliyozinduliwa na kutembelewa ni pamoja na Kituo cha Afya Nyabiyonza, ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita tatu, vyumba 24 vya biashara katika stendi ndogo ya magari Bohari, mradi wa maji Rwamugurusi, mradi wa vijana wa kuchakata taka ngumu (KIUMA), nyumba ya Watumishi Shule ya Sekondari Omurushaka, pamoja na mradi wa uhifadhi wa mazingira na matumizi ya nishati safi na salama.












Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo








