Zaidi ya watu 5,000 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria maonesho ya kuku na ndege yanayotarajiwa kufanyika Oktoba 10 hadi 11, 2025 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
















Akizungumza kuhusu maonesho hayo, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Uzalishaji Vyakula vya Mifugo Tanzania(TAFMA) na Mjumbe wa Kamati inayoandaa Maonesho ya Kuku na Ndege Wafungwa, Sufian Kyarua amesema maonesho hayo yataambatana na mafunzo kwa wafugaji ili kufanya ufugaji wa kisasa.
“Lengo ni kuhakikisha wafugaji wetu wanaongeza ujuzi na utaalamu ili kuhakikisha wanafunga kwa faida na kuhakikisha mazao yao yanakuwa ni salama kwa walaji.
“Haya ni maonesho ya tisa tulianza 2015 tumekuwa tukipata mafanikio kila mwaka hii inaonesha wafugaji wetu pamoja na walaji wanahamu ya kujua bidhaa tunazozalisha."
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo







