KIGODA Cha Uprofesa cha Mwalimu J.K. Nyerere katika Taaluma za Umajumui wa Afrika (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP Centre), limeandaa kongamano kubwa la kujadili Uchumi Jumuishi kuelekea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Kongamano hilo litafanyika Septemba 18, 2025 katika Ukumbi wa Nkrumah Lecture Theatre, Chuo Kikuu Mzumbe – Ndaki ya Mbeya, kuanzia saa 5:00 asubuhi, likiwa na lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali kujadili nafasi na fursa za maendeleo ya taifa.Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mbeya, Mwenyekiti wa Kongamano, Profesa Alexander Makulilo, alisema uhitaji wa kongamano hilo umetokana na kuzinduliwa kwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Julai 17, 2025 jijini Dodoma.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

















