Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) inatarajia kuadhimisha Siku ya unywaji maziwa shuleni mkoani Geita Septemba 24, 2025 katika Viwanja vya Dk. Samia Suluhu Hassan vilivyopo Manispaa ya Geita.
Msajili wa Bodi hiyo, Profesa George Musalya amesema lengo la kupeleka maadhimisho hayo mkoani Geita ni kuhamasisha unywaji maziwa hasa kwa wanafunzi mashuleni ili kuimarisha afya zao.
Aidha,amesisitiza umuhimu wa wazazi kuwahimiza watoto wao kunywa maziwa kwani watakuwa na uwezi wa kufanya vizuri kwenye masomo yao kutokana na virutubishi vilivyopo kwenye maziwa ambavyo vinapatikana kwenye makundi yote ya vyakula.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo




























