Katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Chuo Cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa chuo hicho, Profesa Ahmed Ame, amesema kuna umuhimu mkubwa wa kutumia takwimu katika kutengeneza sera za maendeleo ya taifa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Septemba 1, 2025, wakati wa ufunguzi wa semina kwa waandishi wa habari, Prof. Ame amesema Serikali imepanua wigo wa matumizi ya takwimu katika upangaji wa maendeleo na kusisitiza kuwa takwimu sahihi ndizo msingi wa maamuzi bora.“Takwimu ni namba ambazo haziongopi. Zinawawezesha wananchi kuelewa kwa usahihi kile kinachofanyika,” amesema Prof. Ame.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

















