Askari wa Jeshi la Magereza mkoani Njombe, Erasto Mlelwa (26) amekatiza uhai wake, kwa kujirusha kutoka kwenye gari la polisi na kufa, baada ya kudaiwa kushiriki mauaji ya askari mwenziwe Dickraka Mwamakula (24), huko Lilondo halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma. 

Hayo yamebainishwa Septemba 21, 2025 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga, akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya jeshi hilo, mkoani humo.
Amesema jeshi hilo lilikuwa linaendelea na uchunguzi kufuatia taarifa za kupotea kwa askari Mwamakula, ambaye aliripotiwa kupotea tangu Septemba 7, 2025, mara ya mwisho alikuwa na askari mwenzake Erasto Mlelwa.
Amesema askari hao walielekea eneo moja lililofahamika kwa jina la Lilondo, huko Madaba, kwa ajili ya kuangalia mashamba lakini baada ya hapo, Mwamakula hakuonekana mpaka jeshi la polisi lilipoanzisha uchunguzi wa kina.
Watuhumiwa hao wote wawili, baada ya mahojiano walionesha mwili wa Mwamakula, mahali ulipo ukiwa na majeraha makubwa eneo la kisogoni, lakini mwili wake ukiwa umechomwa moto na kufukiwa katika eneo la mashamba.
Wakati jeshi hilo linaenda hospitali ya Lilondo, kwa ajili ya kumpata daktari ili kufanya uchunguzi wa mwili huo (postmortem) mtuhumiwa Mlelwa, aliamua kujiondoa uhai wake kwa kuruka kutoka kwenye gari na kuangukia kichwa.
Mwili wa marehemu Dickraka umehifadhiwa katika hospitali ya Kibena, kwa ajili ya taratibu zingine za mazishi, lakini mwili wa Mlelwa, upo huko Madaba, kwa ajili ya kusubiri uchunguzi wa daktari.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo










.jpeg)






