Kampuni ya Kitanzania ya JUSTFIT inayojihusisha na uuzaji na utengenezaji wa vifaa vya michezo kwa kushirikiana na Bodi ya Ligu Kuu Tanzania, imezindua mpira wa kwanza wa Ligi Kuu ambao ni mpira rasmi utakaokuwa ukitumika katika msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mpira huo ni ubunifu wa Kitanzania ambao umebeba alama ya ubunifu, upekee na ubora wa hali ya juu kwa viwango vya kidunia ambapo uzinduzi wake umehudhuriwa na Salim Salim ambaye ndiye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JUSTFIT akiwa na Makamu wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi Kuu,Ibrahim Mwayela.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


























