Magazeti leo Septemba 30,2025

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa, pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Hajjat Fatma Mwassa, wameungana na Maaskofu, Mapadri, Viongozi wa Kanisa Katoliki na waumini kushiriki Misa Takatifu ya mazishi ya Hayati Askofu Mkuu Novatus Rugambwa, Balozi wa Baba Mtakatifu.
Misa hiyo Takatifu imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Kardinali Protase Rugambwa, katika Kanisa Kuu Katoliki Jimbo la Bukoba, mkoani Kagera tarehe 29 Septemba 2025.

Viongozi mbalimbali na wanafamilia walishiriki Misa hiyo, akiwemo Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mhashamu Wolgang Pisa; Balozi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Mkuu Angelo Acattino; Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Mhashamu Jovitus Mwijage; pamoja na Mapadri, Watawa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, na waamini kutoka ndani na nje ya mkoa wa Kagera.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news