Kiongozi wa upinzani nchini Uganda,Kizza Besigye amesusia kikao cha kuanza kwa kesi yake, akisema Jaji ambaye anasikiza kesi hiyo anamwonea na analenga kumhujumu.
Besigye amekuwa kizuizini kwa miezi kadhaa, hali ambayo imezua maswali iwapo Rais Yoweri Museveni kwa kweli anazingatia na kuheshimu haki za kibinadamu.
Museveni anasaka kuchaguliwa tena kwenye uchaguzi wa urais ambao utafanyika mnamo Januari mwaka ujao.
Kesi ya Besigye na msaidizi wake Obed Lutale ilipaswa kuanza Jumatatu baada ya kucheleweshwa kwa miezi kadhaa.
Hata hivyo, wawili hao walisusia vikao vya kesi baada ya shinikizo la kumtaka Jaji Emmanuel Baguma ajiondoe kukosa kuzaa matunda.
Jaji Baguma mwenyewe alikataa kujiondoa katika kesi hiyo kwa mujibu wa wakili wa Besigye Eron Kiiza.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

























