Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe , Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amepokea taarifa ya maendeleo ya Chuo Kikuu Mzumbe na kufurahishwa na kasi ya maendeleo iliyofikiwa na Chuo kwa takribani mwaka mmoja tangu alipopokea taarifa ya mwisho mwezi Novemba 2024.
Akipokea taarifa hiyo jijini Dar es Salaam Dkt. Shein amempongeza mwenyekiti wa Baraza la chuo Kikuu Mzumbe Prof. Saida Yahya Othman kwa kuongoza vyema Baraza hilo ambalo ndicho chombo cha juu cha maamuzi na kusema kuwa Baraza limekuwa likisimamia vyema utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Chuo sambamba na kuipongeza Menejimenti nzima na Wafanyakazi ambao ameeleza kuwa wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kukiendeleza Chuo kwa weledi mkubwa chini ya uongozi mahiri wa Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. William Mwegoha.
























