Mavunde aendelea na kampeni mtaa kwa mtaa

DODOMA-Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtumba mkoani Dodoma kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Anthony Mavunde ameendelea na awamu ya kwanza ya kampeni zake za mtaa kwa mtaa kwa kutembelea Kata ya Ihumwa huku akikutana na kuzungumza na wananchi katika mitaa mbalimbali.
Mavunde katika ziara hiyo alitembelea na kufanya mikutano ya kampeni katika mitaa ya Chang’ombe, Chilwana, Ilolo na Ihumwa, ambapo alieleza sera na mikakati yake ya maendeleo kwa wananchi wa Jimbo la Mtumba endapo atachaguliwa kuwa mbunge.
Aidha,pamoja na kueleza dhamira yake ya kuleta maendeleo,Mavunde alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kuwapa kura wagombea wengine wa CCM akiwemo Mgombea Urais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea Udiwani wa Kata ya Ihumwa,Edward Magawa.

Hata hivyo,kampeni hizo zinaendelea katika maeneo mengine ya jimbo hilo, huku Mavunde akiendelea kusisitiza mshikamano, amani na maendeleo kwa Watanzania wote kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news