Ndoa yenye utulivu inajenga msingi imara ndani ya familia na jamii-Katibu Mkuu Abeida

DAR-Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,ndugu Abeida Rashid Abdallah amesema,ndoa yenye sakina (utulivu) inajenga msingi imara ndani ya familia na jamii, hivyo jukumu la kuhamasisha ndoa hiyo ni wajibu wa kila mtu,familia,jamii na viongozi wa kitaifa kwa maendeleo ya taifa.Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ndugu Abeida Rashid Abdallah akizungumza katika kongamano la Utulivu wa Maisha ya Ndoa lenye mada: Siri ya Ndoa yenye Sakina, kongamano hilo limefanyika Septemba 13, 2023, katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na limeandaliwa na Jumuiya ya Khairun Nisaa Foundation.

“Kila mmoja anawajibu wa kuhamasisha ndoa yenye sakina katika kuhakikisha hatua madhubuti za kuimarisha maadili mema yanazingatiwa,sunnah na akhlaq njema;

Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo katika Kongamano la Utulivu wa Maisha ya ndoa lenye mada: Siri ya Ndoa yenye Sakina ambalo limefanyika Septemba 13, 2023 katika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na kuaandaliwa na Jumuiya ya Khairun Nisaa Foundation.
Ndugu Abeida amesema,siri zinazosaidia kuimarisha ndoa yenye baraka na thabiti, ikiwemo ni pamoja na kumcha Allah na kuzingatia mipaka yake,upendo na huruma baina ya wanandoa na mawasiliano na uvumilivu katika changamoto.

Pia, amesema kuheshimiana na kushirikiana katika majukumu ya familia inaleta utulivu katika ndoa.

Aidha,amesema wizara yake inafanya juhudi mbalimbali za kuelimisha jamii kuhusu malezi ya watoto ambayo yanahitaji ushirikiano wa baba na mama kwani yanaleta upendo ndani ya familia.

Amefahamisha kuwa,wizara pekee haitaweza kufanikisha ndoa zisivunjeke,lakini kwa mashirikiano kati Serikali na taasisi binafsi, hata mtu mmoja mmoja anapaswa kushiriki katika kuhamasisha masuala ya malezi bora ya familia.

Vilevile ametoa pongezi za dhati kwa Khairun Nisaa Foundation kwa kuandaa jukwaa hilo la kipekee.

"Ni furaha kuona wanawake na jamii kwa ujumla wakijitahidi kuboresha maisha yao kwa kuelimika na kuhamasisha kuhusu masuala ya ndoa na familia."
Pia ndugu Abeida alimuomba Mwenyezi Mungu awaongoze waumini katika kufuata wingo wa maisha ya ndoa na familia kama alivyokuwa Bibi Aisha (R.A) Mke wa Mtume Muhammad (S.A.W).

Alimalizia kwa kusema familia bora, Taifa imara ni nguzo ya maisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news