MWANZA-Licha ya kuwa tayari timu ya kamba wanawake ya TAKUKURU ilikwisha fuzu hatua ya 16 bora leo Septemba 6, 2025 imeibuka mshindi wa 2-1 dhidi ya timu ngumu ya RAS Tanga.
Pamoja ya kwamba mchezo huo ulikuwa wa kukamilisha ratiba, lakini ulikuwa na ushindani mkubwa kwani timu zote zilikuwa zimelingana alama na hivyo mchezo huo ulikuwa ni lazima apatikane kiongozi wa kundi hili lililokuwa na timu za RAS Tanga, Ofisi ya Makamu wa Rais, TAKUKURU na Wizara ya Mifugo.Mashindano ya SHIMIWI 2025 yanatarajiwa kufunguliwa rasmi na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Septemba 7, 2025 katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza.
Tags
Habari
Michezo
SHIMIWI 2025
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
TAKUKURU Sports Club