Rais Dkt.Mwinyi azindua rasmi majengo ya Mahakama yenye miundombinu ya kisasa

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amezindua rasmi majengo mapya ya Mahakama za Mikoa na Wilaya Mazizini, Mkoa Mjini Magharibi leo Septemba 8,2025.
Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali ina mpango maalum wa kujenga majengo ya Afisi za Serikali, Baraza la Wawakilishi na Mahakama ili kuimarisha uwajibikaji na utoaji wa huduma bora.
Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kukamilika kwa Mahakama hizo ni mwanzo wa mradi mwingine chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia, utakaohusisha ujenzi wa Mahakama tano pamoja na Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa watendaji wa Mahakama kutunza miundombinu hiyo na ameipongeza Mahakama ya Tanzania na Kampuni ya CRJE–East Africa kwa kazi nzuri ya usanifu na ujenzi wa majengo hayo ya kisasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news