ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa majengo mapya ya Mahakama za Mkoa na Wilaya.
Ufunguzi huo utafanyika Septemba 8,2025 saa 2:00 asubuhi katika Viwanja vya Mahakama ya Mkoa, Mazizini huko Mkoa wa Mjini Magharibi.
