ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo 6 Septemba 2025 akiwasili katika Uwanja wa Mao Tse Tung kufungua Michezo ya Majeshi ya Tanzania.
Alipokelewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, CDF Jenerali John Jacob Mkunda pamoja na Viongozi wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama.Michezo hiyo imeandaliwa na Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA).











