RC wa Shinyanga aipongeza Bodi ya Bima ya Amana (DIB)

GEITA-Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (RC),Mheshimiwa Mboni Mhita ametembelea banda la Bodi ya Bima ya Amana (DIB) leo Septemba 22,2025 katika Maonesho ya Nane ya Teknolojia ya Madini ambayo yanayoendelea mjini Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Mboni Mhita, akisaini kitabu cha wageni katika banda la Bodi ya Bima ya Amana (DIB).

Mkuu huyo wa Mkoa ameipongeza DIB kwa kazi inazofanya ambazo ni muhimu katika kuchangia uthabiti wa sekta ya fedha.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Mboni Mhita, akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Umma na Mawasiliano wa DIB, Bw. Lwaga Mwambande, pembeni yake ni Afisa Mwandamizi Mkuu wa DIB, Bi. Kulwa Kasuka.
Katika banda hilo la DIB, Mheshimiwa Mhita  ameelezwa kuhusu majukumu ya bodi ikiwemo kusimamia mfuko wa bima ya amana, kulipa fidia kwa wenye amana iwapo benki au taasisi ya fedha itafungwa na kufilisika, pamoja na kuendesha shughuli ya ufilisi wa benki au taasisi ya fedha inapoteuliwa kufanya hivyo na Benki Kuu ya Tanzania.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ameelezwa kwamba kuanzia Julai mwaka huu, DIB itakuwa na jukumu lingine la kupunguza hasara katika benki au taasisi ya fedha (loss minimiser) ambayo inapitia changamoto katika utendaji wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here