REA kivutio kikubwa uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku

GEITA-Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea kuuza majiko banifu kwa bei ya ruzuku katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan, Bombambili mkoani Geita.
Katika maonesho ya madini, REA inauza majiko banifu kwa gharama ya shilingi 6,200 tu ambapo kabla ya ruzuku kutolewa na Serikali majiko hayo yaliuzwa kwa gharama ya shilingi 41,300.
Majiko banifu yametengenezwa kwa teknolojia ya kisasa yenye uwezo wa kupunguza sumu ya mkaa (carbon monoxide) hivyo kusaidia kupunguza madhara ya kiafya yatokanayo na nishati ya mkaa.

Katika mkoa wa Geita kampuni inayosambaza majiko banifu kwa bei ya ruzuku ni Geita Millenium Star Company Limited.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news