Selfie ya Oktoba Tunatiki:Chagua Dkt.Mwinyi, kiongozi mwenye maono na uongozi wa kweli

ZANZIBAR-Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameendelea na kampeni zake Zanzibar, huku akiendelea kuwaeleza wananchi kuhusu yajayo yatakavyoleta neema zaidi Zanzibar.
Kwa msingi huo,tuungane kwa pamoja na Mama Maria Mwinyi kwenda kupiga kura Oktoba ili kumrejesha Dkt.Mwinyi aendelee kuleta mabadiliko ya kweli kwa nchi yetu, huyu ni kiongozi mwenye maono na uongozi wa kweli.

Hivyo, chagua Dkt.Mwinyi na CCM kwa maendeleo endelevu, amani, na ustawi wa taifa letu. Kiongozi anayejali mustakabali wa wananchi na ambaye ana dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko makubwa kwa kila sekta Zanzibar.

Dkt.Mwinyi ni kiongozi anayefahamu mahitaji ya watu na ni mzalendo ambaye amejiandaa kuja kuendeleza mambo mazuri yaliyofanyika katika miaka mitano, na kutekeleza miradi mipya kupitia #UongoziUnaoachaAlama. Kwa sasa,hakuna mwingine anayeweza kutoa alama hiyo kama Dkt.Mwinyi.

Kwa pamoja, tutajivunia mafanikio ya nchi yetu, kwa ajili ya watoto wetu na vizazi vijavyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news