Simba SC yasitisha mkataba wa kocha mkuu Fadlu Davids

DAR-Klabu ya Simba SC imethibitisha umefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha Mkuu Fadlu Davids kama kocha mkuu klabuni hapo na kubainisha kwamba makubaliano hayo ni matakwa binafsi ya kocha Fadlu kwa uongozi wa klabu hiyo.
Simba SC imethibitisha hilo kupitia taarifa yake kwa umma ya leo Septemba 22, 2025 huku ikimshukuru kocha huyo kwa kuiongoza klabu hiyo kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na kumalizia nafasi ya pili kwenye Ligi kuu ya NBC.

Aidha,uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi umemtakia heri na baraka kocha Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini katika maisha yake ya soka nje Simba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here