MTWARA-Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Wilaya ya Tandahimba imekabidhi shilingi 500,000 kwa Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Salama, Mwalimu Mustafa Shaibu Rashidi, iliyookolewa na TAKUKURU baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Mkupete wilayani humo katika mkutano wa hadhara uliofanyika mwezi Aprili,2025.
Ilielezwa kwenye mkutano huo kwamba wananchi hao walichanga fedha kwa ajili ya kumlipa mwalimu wa somo la Biology na Elimu ya Dini ya Kiislam katika Shule ya Sekondari Salama iliyopo kijijini hapo, lakini Mwalimu Lameck Sijaona Kijalo ambaye alikuwa akisimamia ukusanyaji huo, alizitumia fedha hizo kwa manufaa yake binafsi.
Fedha hizo zimekabidhiwa leo Septemba 4,2025 katika Shule ya Sekondari Salama na Afisa wa TAKUKURU, Bi. Siudhiki Mohamed Joginda, mbele ya wananchi wa Kijiji cha Mkupete.
