TBS yaendelea kuwashika mkono wajasiriamali wadogo nchini

NA GODFREY NNKO

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limesema kuwa, limeendelea kutenga zaidi ya shilingi milioni 350 kila mwaka kwa ajili ya kuhudumia wajasiriamali wadogo na wa kati pale wanapoomba bidhaa zao wanazozizalisha wenyewe zithibitishwe ubora.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt. Ashura Katunzi ameyasema hayo leo Septemba 18,2025 katika kikao kazi kati ya wahariri na waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari nchini chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Dkt.Katunzi amesema kuwa,wamekuwa wakitoa huduma hiyo kwa wajasiriamali kutokana na mahitaji na wataendelea kuwahudumia kadri inavyowezekana katika halmashauri zote nchini.
Pia,amesema, wataendelea kuwasiliana na watendaji katika halmashauri mbalimbali nchini ili kuweza kuwatambua wajasiriamali ambao wana bidhaa zao na wanatamani ziwe katika viwango bora,lakini hawana uwezo ili ziweze kupata soko la ndani na nje.

"Tutaendelea kuwahudumia wajasiriamali wadogo ili kuhakikisha wanazalisha kilicho bora kwa soko la ndani na nje."

Vilevile amesema, kupitia maabara 12 za TBS ambazo zimehakikiwa na kupewa vyeti vya ithibati ya Kimataifa zimeendelea kuwasaidia watengenezaji bidhaa kuongeza na kuimarisha ubora wa bidhaa zao.
Pia, zinasaidia kupimia bidhaa ili kuhakikisha zinafaa kwa matumizi yaliyokusudiwa na kuhakikisha ubora wa bidhaa kabla ya kusafirishwa nje ya nchi au kuingizwa nchini.

"Gharama za kutokupima bidhaa ni kubwa kuliko gharama za kupima bidhaa,"amesisitiza Dkt.Katunzi huku akihimiza wazalishaji na waingizaji wa bidhaa kufuata taratibu zilizowekwa na Serikali kupitia TBS.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news