GEITA-Viongozi mbalimbali wametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania katika Maonesho ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea mkoani Geita, na kujionea namna wataalamu wa Benki Kuu wanavyotoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yake.
Elimu hiyo imejikita katika kueleza majukumu ya Benki Kuu ikiwemo kudhibiti mfumuko wa bei, kusimamia mabenki na taasisi za kifedha, pamoja na kulinda thamani ya shilingi ya Tanzania.Miongoni mwa viongozi waliotembelea banda hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Mhe. Abdallah Komba, Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe. Grace Kingalame, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Dkt. Janet Lekashingo, pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita (RMO), Dkt. Omari Sukari.






