MWANZA-Katika hatua ya kuwatia moyo, Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza, Bw. Abnery Mganga ametembelea washiriki wa TAKUKURU SPORTS CLUB waliopo katika viwanja vya michezo vya Shule ya Sekondari Bwiro Wavulana, ambako mashindano yanafanyika.
Bw. Mganga amewapongeza kwa hatua nzuri iliyofikiwa, lakini pia aameeleza kuwa, TAKUKURU Mkoa wa Mwanza itaendelea kutoa ushirikiano muda wote kwenye kila jambo ili kuhakikisha timu za TAKUKURU zinafanya vema kwenye SHIMIWI 2025.
Pia,amewataka wachezaji waendelee kujituma na kuendeleza mazoezi ili kuleta ubingwa na kuwa mfano wa kuigwa katika nidhamu ili kujenga taswira chanya ya TAKUKURU
Vilevile, Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza amewataka watumishi hao kundeleza mapambano hadi kuchukua ubingwa wa taifa.
