Yanga SC yaongoza kwa utajiri barani Afrika

NA DIRAMAKINI 

MWENYEKITI wa Kamati ya Mabadiliko ya Mfumo wa Uendeshaji wa Young Africans Sports Club (Yanga SC), Alex Mgongolwa amesema,kwa sasa thamani ya klabu hiyo imefikia shilingi bilioni 100 (zaidi ya dola milioni 40).
Mgongolwa ameyasema hayo leo Septemba 7, 2025 katika mkutano mkuu wa klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam.

Pengine thamani hii ya Yanga SC ni kubwa zaidi kwa siku za hivi karibuni barani Afrika ikifuatiwa na Mamelodi Sundowns Squad ya Afrika Kusini ambayo thamani yake ni dola za Kimarekani milioni 39.7 (zaidi ya shilingi bilioni 90).

Aidha, Al Ahly SC Squad thamani yake inakadiriwa dola milioni 37.21,Orlando Pirates ya Afrika Kusini yenye thamani ya dola za Marekani milioni 24.95,Pyramids FC yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 23.7.

Esperance de Tunis ya Tunisia thamani ya dola za kimarekani milioni 22.3,Zamalek SC ya Misri thamani ya dola milioni 22,Wydad Casablanca ya Morocco yenye thamani ya dola milioni 21.7 mtawaliwa.
"Nichukue nafasi hii kuwaambia rasmi wanachama wa Yanga, thamani ya timu yetu imefikia shilingi bilioni 100," amesema Mgongolwa.

Mgongolwa amezungumza hayo baada ya kupewa nafasi na Rais wa Yanga, Injinia Hersi Saidi kwa ajili ya kutoa ripoti ya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo.

Katika mkutano wa leo, umehudhuriwa na jumla ya wanachama 627 kutoka katika matawi mbalimbali 163 ya timu hiyo.

Mkutano huo ukiwa ni wa mikakati mipya ya klabu hiyo kwa msimu mpya wa mashindano wa mwaka 2025-2026 ikiwa ina kazi ya kutetea mataji ya Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho, Ngao ya Jamii na Kombe la Muungano, lakini ikiwa na kibarua cha Ligi ya Mabingwa Afrika.
Yanga imepangwa kuanza mechi za raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Wiliete Benguela ya Angola siku chache baada ya kumalizana na Simba katika Ngao ya Jamii itakayochezwa Septemba 16.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here