Aliyekuwa Mlinzi Mkuu ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera hatiani kwa rushwa

KAGERA-Aliyekuwa Mlinzi Mkuu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera,Bw.Warioba Nzwili Sayi ametiwa hatiani kwa makosa ya rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba mkoani humo.
Sayi ametiwa hatiani Oktoba 6,2025 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Bukoba, Mheshimiwa Janeth Massesa kupitia shauri la Rushwa namba 24339/2025.

Chini ya kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, ilidaiwa mshtakiwa huyo kwa njia ya rushwa alijipatia kiasi cha 4,000,000 kutoka kwa Emiliana Jema Shibumbila ili aweze kumpatia mtoto wake ajira.

Ni baada ya mlinzi Warioba Nzwili Sayi kujifanya kwamba yeye ni Afisa Utumishi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Baada ya mshtakiwa kutiwa hatiani ametakiwa kulipa faini ya shilingi 500,000 au kwenda jela mwaka mmoja na kutakiwa kurejesha kiasi cha shilingi 4,000,000 alichojipatia kwa njia ya rushwa kwa mlalamikaji Bi.Emiliana Shibumbila ndani ya miezi mitano.

Aidha,mshtakiwa amelipa faini ambapo shauri hilo liliendeshwa na waendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera, Wakili William Fussi na Daudi Jacob Oringa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news