NA DIRAMAKINI
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeshiriki katika Soko la Jumla la Fedha za Kigeni (Interbank Foreign Exchange Market-IFEM) kwa mujibu wa Sera ya Ushiriki katika Soko la Fedha za Kigeni ya Mwaka 2023.
Katika utekelezaji wa sera hiyo, BoT imeuza jumla ya Dola za Marekani milioni 20 kupitia mnada wa ushindani, kwa kiwango cha wastani cha Shilingi 2,465.13 kwa Dola moja ya Marekani.
Ushiriki huu unalenga kuimarisha na kuongeza ukwasi katika soko la fedha za kigeni, sambamba na kuhakikisha uthabiti wa thamani ya Shilingi ya Tanzania na uendelevu wa miamala ya biashara ya kimataifa.
Aidha,hatua hii ni sehemu ya juhudi endelevu za Benki Kuu kudhibiti mienendo ya soko la fedha za kigeni na kuweka mazingira bora ya kifedha yanayochochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

