Dkt.Mwinyi,Mama Mariam Mwinyi wasisimua Pemba:Waacha msafara,wajiunga na wananchi kununua matunda

ZANZIBAR-Mgombea wa nafasi ya Rais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akiwa ameambatana na mke wake Mama Mariam Mwinyi, wamesimama njiani kununua matunda aina ya Mabungo wakitokea Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, baada ya mkutano wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), katika mwendelezo wa kampeni zake leo Oktoba 7,2025.
Tukio hilo limevutia hisia za wananchi waliokuwa kandokando ya barabara, ambapo wengi walionesha furaha na kupongeza unyenyekevu wa viongozi hao, waliokuwa wakijumuika nao katika shughuli za kawaida za maisha ya kila siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news