Dkt.Natu Mwamba ateta na Mkurugenzi wa IMF anayesimamia Idara ya Afrika

WASHINGTON-Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Mhe. Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anayesimamia Idara ya Afrika, Bw. Abebe Selassie makao makuu ya taasisi hiyo jijini Washington D.C nchini Marekani.
Pamoja na mambo mengine amempa sifa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kusimamia vema sera za uchumi na fedha za nchi yake ikiwemo kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na namna anavyosimamia fedha za miradi zinazotolewa na Taasisi hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika.

Bw. Abebe alisema kuwa, Tanzania ni nchi ya mfano katika usimamizi wa sera za uchumi na fedha ambapo licha ya changamoto za UVIKO 19 na mizozo ya kisiasa inayoendelea sehemu mbalimbali duniani, tathimini ya Shirika hilo inaonesha kuwa uchumi wa Tanzania uko imara ikilinganishwa na nchi nyingine nyingi za Afrika.
Katika Mkutano huo Dkt. Mwamba aliishukuru IMF kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya nchi kupitia misaada, mikopo nafuu na misaada ya kiufundi pamoja na miongozo mbalimbali inayoipatia nchi hatua iliyosaidia kuimarisha uchumi wa nchi.

Tanzania ni mwana hisa wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia na ushiriki wake katika mikutano hiyo unalenga kulinda na kutetea maslahi ya nchi katika mashirika hayo makubwa ya fedha duniani kwa kushiriki mikutano ya kiutawala na kiuendeshaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news