SINGIDA-Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba ameunga mkono kampeni ya kununua jezi halisi (original) za timu ya Simba SC, akitoa rai kwa wapenda soka wote kuepuka jezi bandia (feki).
Amesema,jezi feki zinaikosesha timu mapato muhimu kwa ajili ya usajili wa wachezaji bora, na pia zinaikosesha serikali mapato ya kodi.
Ameyasema hayo nyumbani kwake Misigiri Iramba mkoani Singida, alipotembelewa na ugeni wa timu ya mauzo ya simba ukiongozwa na Msemaji wa Timu hiyo Ahmed Ally.















