MBEYA-Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Bi. Mary Maganga, ametembelea mabanda ya Maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa, ikiwemo banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu katika maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa 2025 yanayofanyika katika viwanja vya Uhindini jijini Mbeya leo Oktoba 9,2025.
Maadhimisho haya yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Nguvu Kazi ya Vijana kwa Maendeleo Endelevu.”



