DODOMA-Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri ameelekeza kazi kufanyika kwa kuzingatia Sheria, Taratibu, Kanuni na Miongozo ya Utumishi wa Umma.
Amesema hayo katika kikao na watumishi wa Idara ya Utawala, Wizara ya Maji.
Mhandisi Mwajuma amesisitiza suala la kuzingatia mabadiliko na kutoa majibu kwa watumishi wa umma wanapokwama katika masuala mbalimbali.


