MKUU wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala amemuagiza Mkandarasi M/s Serengeti Limited anayetekeleza mradi wa ujenzi wa Mradi wa Uendelezaji Miji Tanzania (TACTIC) katika Manispaa ya Mtwara Mikindani, kukamilisha kazi hiyo kwa wakati na ubora uliokusudiwa kwa mujibu wa Mkataba ili wananchi waanze kunufaika na miundombinu hiyo inayotekelezwa mkoani humo.
Kanali Sawala ametoa maagizo hayo Oktoba 10, 2025 mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mradi huo unaohusisha uboreshaji wa miundombinu ya barabara za Chuno na Samia City, mitaro ya kutiririsha maji ya Mvua eneo la Kiyangu, ujenzi wa Kituo kikuu cha mabasi eneo la Chipuputa, Kituo cha wajasiriamali eneo la Skoya pamoja na jengo la usimamizi, mradi utakaogharimu jumla ya shilingi Bilioni 27.49.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


























