Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema hali ya usalama katika jiji hilo inaendelea kuwa shwari, huku shughuli za kiuchumi, kijamii na kisiasa zikiendelea kwa utulivu.Pia,jeshi hilo linawashikilia watu wanne kwa kosa la kuendesha televisheni mtandao bila kufuata sheria.
Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 15,2025 kamanda wa polisi kandaa maalim Jumanne Murilo amesema wananchi wanaendelea kushiriki katika mikutano ya vyama vya siasa, na wagombea wote wapo salama, jambo linaloonyesha hali nzuri ya amani na usalama katika kipindi hiki cha kampeni.









Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo















