Polisi katika Kaunti ya Homa Bay wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa cha kuteketezwa kwa nyumba ya Mbunge wa Rangwe, Dkt.Lilian Gogo katika Kijiji cha Kotieno usiku wa Ijumaa.

Nyumba hiyo iliteketezwa kwa moto, wakati mbunge huyo akishughulikia mipango ya mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Amolo Odinga,akiwa mwanachama wa Kamati ya Kitaifa ya Mazishi.“Tumeondoa uwezekano wa hitilafu ya umeme. Moto huu ulisababishwa na mtu aliyeuwasha kwa makusudi,” alisema Kamanda Chebet.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
















