Umoja wa Kitaifa wa Asasi za Kiraia wa Shule Salama (NSSC) umetoa rai kwa vyama vya siasa na wagombea nchini kuepuka kuwatumia wanafunzi na watoto katika kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ukisisitiza kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa haki za watoto na kinyume cha sheria.
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, wanachama wa umoja huo wamesema kumekuwepo na matukio ya wanafunzi kutolewa darasani kushiriki mikutano ya kampeni, hali ambayo ni hatari kwa usalama, ustawi na haki ya mtoto ya kupata elimu.Mkuu wa Idara ya Utafiti, Ubunifu na Uchambuzi wa Sera wa HakiElimu, Bw. Makumba Mwemezi, aliyemuwakilisha Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, amesema ni wajibu wa asasi za kiraia kulinda watoto hususan katika kipindi hiki cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo












