Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu ambaye pia ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM), Profesa Mussa Juma Assad, amesema hali ya uchumi wa Tanzania imeimarika katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Profesa Assad ameyasema hayo mjini Morogoro katika Kongamano la Kitaaluma la kujadili Utekelezaji wa Uchumi Jumuishi kufikia Dira 2050, lililoandaliwa na Chuo kikuu MUM kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC).Amesema kwa vigezo vya kiuchumi, Tanzania inaendelea kufanya vizuri ukilinganisha na baadhi ya nchi jirani kama Kenya na Rwanda, ambapo ukuaji wa pato la taifa (GDP) umeendelea kuwa thabiti.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo




















