Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza Oktoba 29, 2025 ambayo itakua ni siku ya Uchaguzi Mkuu kuwa ni Siku ya Mapumziko kwa Wananchi wote.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa Oktoba 24,2025 na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka ambapo ameeleza kuwa, uamuzi huo unalenga kuwapa nafasi Wananchi wote wenye sifa kwenda kupiga Kura ili kutekeleza wajibu wao wa Kidemokrasia.Dkt.Samia amewasihi wananchi wote kufuata maelekezo na miongozo iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ili kuhakikisha zoezi la upigaji kura linafanyika kwa amani,utulivu na nidhamu kama ilivyo desturi ya Taifa letu.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo











.jpeg)






