Magazeti leo Oktoba 8,2025

WILAYA  Mafia mkoani Pwani imesisitiza ushindani huru katika soko la mwani ili kumnufaisha mkulima, kuinua pato pamoja na kukuza uchumi wa wilaya hiyo.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka wa fedha 2024/2025, mavuno ya mwani yalifikia tani 600 zenye thamani ya sh.milioni 420, kwa bei ya wastani ya Sh.700 kwa kilo.

Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Aziza Mangosongo, anasema serikali inaruhusu ushindani wazi wa wanunuzi wa mwani kwa kuzingatia sheria na miongozo iliyopo, bila kuwepo kwa ukiritimba , ama mnunuzi mmoja au kampuni.

Mangosongo aliyasema hayo Oktoba 6, 2025, katika kikao kilichowakutanisha wadau wa kilimo cha mwani wilayani humo, kilicholenga kujadili na kutafuta suluhisho kwa baadhi ya changamoto zinazowakabili wakulima hao ikiwemo uwepo wa mnunuzi mmoja mkubwa, kampuni ya Mwani Mariculture, anayehodhi soko kwa sasa.

“Sisi kama Mafia tunaenda na azimio la kufungua milango kwa wanunuzi wengine kuingia sokoni, tunataka taratibu zifuatwe na kila kitu kinachowahusu wakulima kipitie halmashauri ili Idara ya Kilimo iwe na taarifa sahihi,” alielezea Mangosongo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news