Naibu Waziri Chumi ateta na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela

KAMPALA-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Cosato Chumi amekutana na kuzungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela anayeshughulikia Masuala ya Afrika, Mhe. Yuri Pimentel.
Mazungumzo hayo yamefanyika pembezoni mwa Mkutano wa 19 wa Mawaziri wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM) unaofanyika Kampala, Uganda kuanzia tarehe 13 hadi 16 Oktoba 2025.
Viongozi hao wamejadili namna ya kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Venezuela hususan katika kukuza biashara, uwekezaji na utalii.

Venezuela inakamilisha taratibu zake za ndani ili kufungua Ubalozi wao nchini Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news